Home » ESTHER MUSILA   » Roho Yangu by ESTHER MUSILA Feat. GUARDIAN ANGEL

Roho Yangu by ESTHER MUSILA Feat. GUARDIAN ANGEL

Bwana Mungu nashangaa kabisa
Nikifiki jinsi ulivyo
Nyota ngurumo vitu vyote pia
Viumbavyo kwa uwezo wako

Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu

Nikitembea kote duniani
Ndege muimba nawasikia
Miliamia hupendeza macho sana
Upepo nao nafurahia 

Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu

Nikikumbuka vile wewe Mungu
Ulivyompeleka mwanao
Afe azichukue dhambi zetu
Kuyatambua ni ngumu mno

Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu

Yesu Mwokozi utakaporudi
Kunichukua kwenda mbinguni
Nitaimba sifa zako milele
Wote wajue jinsi ulivyo

Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu
Roho yangu na ikuimbie
Jinsi wewe ulivyo mkuu